Magaidi watano waangamizwa nchini Misri

Magaidi watano waangamizwa nchini Misri

Wizara ya mambo ya ndani nchini Misri imetangaza kuangamia kwa magaidi watano nchini humo kufuatia mashambulizi makali yaliotokea baina ya majeshi ya usalama ya Misri na vikundi vya kigaidi sehemu ya Suhaji nchini humo.

Shiriuka la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Wizara ya mambo ya ndani nchini Misri imetangaza kuangamia kwa magaidi watano nchini humo kufuatia mashambulizi makali yaliotokea baina ya majeshi ya usalama ya Misri na vikundi vya kigaidi sehemu ya Suhaji nchini humo.
Majeshi ya ulinzi na usalama ya Misri yamefanya mashambulizi katika maeneo yanayokaliwa na magaidi katika miinuko iliopo katika barabara ya Syhaji na kufanikiwa kuwaangamiza magaidi watano, na kuteka selaha na vifaa vingine vya kivita.
Inasemekana kwamba majeshi ya Misri yalianza kufanya mashambulizi makali dhidi ya vikundi vya kigaidi nchini kufuatia amri iliotolewa na Rais wa nchi hiyo iliotolewa mwezi wa pili mwaka huu, ambapo aliyataka majeshi hayo kufanya mashambulizi makali dhidi ya magaid na vikundi viliokuwa na silaha katika maeneo ya jangwa la Sinai nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky