Magaidi watatu waangamia kufuatia majeshi ya Misri

Magaidi watatu waangamia kufuatia majeshi ya Misri

Majeshi ya ulinzi na usala ya Misri katika shambulizi liliofanya kaskazini mwa jangwa la Sinai, limefanikiwa kuwaangamiza magaidi watatu wa kikundi potovu cha Takfiri

Shirika la habari Ahlulabayt (a.s) ABNA: Misri yatangaza habari ya kuangamia kwa magaidi wa Takfiri nchini humo, kwa mujibu wa ripoti ya majeshi ya ulinzi na usalama nchini Misri, kwa majeshi hayo yalifanya shambulio maalumu kaskazini mwa jangwa la Sinai na kufanikiwa kuwaangamiza magaidi watatu wa kikundi cha Takfiri.
Kufuatia shambulio hilo wanajeshi wawili wa Misri pia wamejeruhiwa, jangwa la Sinai ndio sehemu ambapayo kikundi cha kigaidi cha Daesh wameifanya kuwa ndio sehemu ya mafichio yao, ambapo sehemu hiyo katika miaka iliopita kulijiri mapambano makali katika ya majeshi ya Misri na magaidi hao, ambapo mpaka sasa mamia ya wanajeshi wa Misri wamepoteza maisha katika shemu hiyo.
Harakati za kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Misri, zilianza miaka mitatu iliopita, ambapo toka kipindi hicho mpaka sasa walishakuwa wamefanya matukio mengi ya kigaidi katika sehemu mbali mbali nchini humo na kupelekea vifo vya mamia ya wananchi wasiokuwa na hatia na wanajeshi wa nchi hiyo.  
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky