Magaidi watatu wakamatwa nchini Libya

Magaidi watatu wakamatwa nchini Libya

Wizara ya mambo ya ndani ya Libya imetangaza kuwakamata magaidi watatu katika kituo kimoja cha ukaguzi nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kiongozi mmoja katika wizara ya mambo ya ndani nchini Libya amesema kuwa magaidi watatu wamekamatwa katika kituo kimoja cha ukaguzi nchini humo.
Aidha “Ahmad Muitiqi” ni mmoja miongoni mwa wanakamati ya uongozi wa Libya amesema, magaidi hao watapewa adhabu kali kwa sababu wamekuwa wakihatarisha amani na usalama na umoja wa kitaifa nchi humo.
Kadhalika amesisitiza kuilinda serika ya umoja wa kitaifa kwaajili ya kuleta amani nchini humo na kuendeleza mapambano dhidi ya vikundi vya kigaidi nchini humo hata kuvisambaratisha vikundi hivyo.
Wizara ya mambo ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya imezitaka sekta zote za usalama kuwa wakae mkao wakula kwaajili ya kukabiliana na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky