Mwanajeshi wa Misri auuliwa kusini mwa Al-arish

Mwanajeshi wa Misri auuliwa kusini mwa Al-arish

Mmoja kati ya wanajeshi wa jeshi la Misri amiuwawa kufuatia kuripuka kwa bomu liliokuwa limetegwa katika njia ya kupita magari ya kijeshi

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: televishen ya Al-jazirah limetangaza kuuwawa kwa mwanajeshi mmoja wa jeshi la Misri na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia mripuko wa bomu uliotokea katika njia ambayo majeshi hayo yalikuwa yakipita kusini mwa Al-arish katika mkoa wa Sinai.
Aidha kuhusu tukio hilo mpaka sasa ufafanuzi bado hujapatikana, kwa upande mwingine hapo awali msemaji wa majeshi ya Misri alitangaza kuwa watu 71 waliokuwa na silaha wameuliwa toka kuanzia awali ya mwaka huu wa 2018, katika mashambulizi mbalimbali yaliofanywa na majeshi hayo katika jangwa la Sinai
Kwa mujibu wa ripoti hii msemaji huyo amesisitiza kuwa: katika mashambulizi hayo, wanajeshi saba wa Misri wameuwawa katika jangwa hilo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky