Sheikh Zakizakiy aripotiwa kuwa na hali mbaya katika jela za Naigeria

 Sheikh Zakizakiy aripotiwa kuwa na hali mbaya katika jela za Naigeria

Vyanzo makini viliopo karibu na familia ya Sheikh Zakizakiy kiongozi wa harakati ya Kiislamu Naigeria vimetoa ripoti ya kwamba hali ya Sheikh Ibrahim Zakizakiy anazidi kuwa mbaya

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: baadhi ya vyanzo makini viliopo karibu na familia ya Sheiukh Zakizakiy “kiongozi wa harakati ya Kiislamu Naigeria” ambaye bado yupo katika jela za serikali ya Naigeria, imeripotiwa hali ya mwili wake kuwa mbaya katika jela hizo, jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa khofu kwa familia yake na wafuasi wake kwa ujumla.
Kwa upande mwingine “Yunusu Abubakari” mwandishi na mchambuzi wa masuala ya Naigeria amesema: Sheikh Ibrahim Zakazakiy ni lazima aachiwe huru, kinyumi na hivyo nchi na jamii  kwa ujumla haitakuwa na kupata maendeleo, kwa maana viongozi wanapaswa kuangalia haki za wananchi za kukosoa na kuacha kuwahujumu pale wanapotoa hisia na mitazamo yao.
Aidha Ibrahim Musa, msemaji mkuu wa kikundi cha harakati ya Kiislamu Naigeria amesema kuwa: Sheikh Zakizakiy anahitaji uangalizi wa hali ya juu wa Daktari kwa haraka, ili asipatwe kiarusi cha Ubongo kwa mara nyingine.
Ibrahim Musa  amesisitiza kwa kusema akiitaka serika li ya Naigeria kumuachia huru Sheikh Zakizakiy kwaajili ya kupata matibabu ya haraka.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky