Siku ya Quds mjini Dar es Salam Tanzania + picha

Siku ya Quds mjini Dar es Salam Tanzania + picha

Katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani Imam Khomeini iliita siku hiyo kuwa ni siku ya kimataifa ya kuwatetea waislamu wa Papalestiana na kibla cha kwanza cha Waislamu iliofahamika kama siku ya (Quds), hivyo waislamu wa Tanzania nao wamejitokeza kwa wingi katika kuadhimisha siku hiyo wakimpinga dhulma wanayofanyiwa wapastina na serikali ya kivamizi ya Israel

Shirika la habari Ahlulbayt (a.s) ABNA: katika ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni siku ambayo Imam Khomein aliita siku hiyo kuwa ni siku ya kimataifa ya Quds ambayo imewekwa kwaajili ya kupinga uvamizi wa Kizayuni dhidi ya Palestina na wapalestina, hivyo waislamu wa Tanzania nao wamejumuika na waislamu wenzao duniana katika kupinga dhulma hizo nchini humo.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika mji wa Dar es Salam ambao ni katika miji mikubwa nchini Tanzania, ambapo waislamu nchini humo walifanya matembezi ya zaidi ya kilometa 4 kwaajili ya kuonyesha hamasa zao za kuwatetea wananchi wa Palestina kutokana na dhulma wanazofanyiwa nchini humo.
Inasemekana kwamba ukiacha maandamano ya mji huo, miji mingine ya nchi hiyo imeonekana kuadhimisha siku ikwemo Arusha Tanga ...hii ni katika hali ambayo inasemekana kuwa Rais mpya wa nchini yuko katika juhudi ya kukuza fungamano lake na serikali ya kivamizi ya Iserael kwa anuani ya kuwa ni taifa linalojitegemea.
Maadamano hayo yamehudhuria na viongozi mbalimbali wa dini na wanasiasi ikiwemo mwanasiasa maarufu Mh Profesa Ibrahim Lipumba pia waliodhuria vingozi wa ubalozi wa Iran nchini Tanzania, mwakilishi wa Jamiatul Mustwafa nchini Tanzania na kiongozi wa kituo cha utamaduni wa Iran, ambapo baada ya kufanya maandamano hayo waislamu walikusanyika katika msikiti (Alghadiri) na kusali Sali sala Ijumaa ikiongozi na Imam wa msikiti huo (sheikh Hemedi Jalala).

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky