Utalii Halali katika mji wa Cape Town, Afrika Kusini

Utalii Halali katika mji wa Cape Town, Afrika Kusini

Mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini unatekeleza sera za kuwavutia watalii wa tamaduni na dini mbali mbali na kwa msingi huo kuna mpango maalumu wa kuwavutia watalii Waislamu katika fremu ya Utalii Halali.

Mji wa Cape Town kama miji mingine ya Afrika ina historia ndefu ya Uislamu ambao umekuwa na taathira chanya katika tamaduni za wenyeji. Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye kuwavutia watalii wengi barani Afrika ambapo mwaka 2016 nchi hiyo ilitembelewa na watalii milioni 1.52. Hivi sasa mji wa Cape Town unapanga mikakati maalumu ya kuwavutia watalii Waislamu.

Kwa mujibu wa taasisi ya Crescent Rating, miongoni mwa maeneo yaisyo ya Kiislamu, Afrika Kusini ni nchi ya nne mashuhuri ya watalii Waislamu.

Enver Duminy, Mkurugenzi wa Baraza la Utalii Cape Town, amesema ingawa mji huo unatazamwa kuwa ni mji wenye wakazi wazungu na Waafrika wachache, sasa kuna mkakati wa kuwavutia watalii Waislamu hasa kwa kuzingatia kuna historia ndefu ya Waislamu mjini humo.

Kwa mfano Hoteli ya Hilton Cape Town imepanua huduma zake kuwavutia wasafiri Waislamu. Mbali na kuwapa wageni miswala na nakala za Qur'ani Tukufu wanapowasilisha ombi, vymba pia vina alama za kuonyesha qibla. Halikadhalika bafu zimejengwa kwa mujibu wa ustaarabu wa Waislamu. Halikadhalika hoteli zenye huduma kamili za utalii Halali haziuzi pombe na nyama ya nguruwe.

Halikadhalika mjini Cape Town kuna migahawa kadhaa inayomilikiwa na Waislamu ambayo inauza chakula halali kwa wasafiri. Halikadhalika mji huo una misikiti kadhaa huku msikiti mkubwa zaidi ukiwa Masjid Gatesville.
..............
300


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky