Wanane wauwawa katika mripoko wa kigaidi uliotokea katika msikiti mmoja Nigeria

Wanane wauwawa katika mripoko wa kigaidi uliotokea katika msikiti mmoja Nigeria

Katika shambulio hilo la kigaidi mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa bomu alijiripua katika msikiti mmoja uliopo katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa mashariki ya Nigeria na kusababisha kuuwawa watu wanane na kujeruhiwa wengine 15

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mwanamke mmoj  aliyekuwa amevaa bomu alijiripua asubuhi ya Jumatatu baada ya sala ya Asubuhi katika msikiti mmoja uliopo katika mji wa Maiduguri nakusabisha vifo vya watu wanane na wengine 15.
Shirika la habari la Ufaransa limetangaza habari hii na kuongeza kusema kuwa wakazi wa mji huo walianza kuwa na mashaka na harakati za mwanamke huyo nadipo wakawa wanamfuatilia mwanamke huyo, na alipofika karibu na msikiti huo walimwambia asimame ili wajiridhishe na mashaka yao, ndipo mwanamke yule hakusimama na akakimbilia msikitini na kujiripua akiwa ndani ya msikiti huo.
Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi mkuu wa masuala ya ukozi na mambo ya dharura kuwa: muda uliokuwa linatokea tukio hilo, wanawake wengine 3 waliokuwa wamevaa mabomu walikutwa katika mji huo ambapo wawili kati yao waliuliwa katika sehemu ya Mamanti na alijiripua katika sehemu nyingine.
Baadhi ya vyombo vya habari vinaeleza kuwa hili ni tukio la pili la kigaidi kutokea ndani ya wiki moja ambapo wanawake 4 waliokuwa wamevaa mabomu, wamefanya matukio hayo yaliopelekea kuuwawa kwa wananchi wasiokuwa na hatia nchini Nigeria.
Siku ya Jumatatu ya wiki iliopita kilitokea mripuko wa kigaidi katika mji wa Maiduguri tukio ambalo lilipelekea kuuwawa watu 19 na kujeruhiwa wengine 23 nchini humo, ambapo kikundi cha kigaidi cha Boko Haram nchini humo hivi karibuni kimeanza kuwatumia wanawake katika kufanya miripuko ya kigaidi nchini Nigeria.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky