Watu 38 na 18 kujeruhiwa kufuatia shambulio la Al-shabab kwa majeshi ya Somalia

Watu 38 na 18 kujeruhiwa kufuatia shambulio la Al-shabab kwa majeshi ya Somalia

Kikundi cha kigaidi cha Al-Shabab chashambulia majeshi ya Somalia na kusababish kuuwawa kwa wanajeshi 38 na kujeruhiwa 18 miongoni mwa majeshi hayo

Shirika la habari AhlulBayt (a.) ABNA: magaidi wa Al-Shabab asubuhi ya Alhamisi wamefanya mashambulizi makali nchini humo dhidi y majeshi ya Somalia katika sehmu ya Puntland nchini humo na kuuwa wanajeshi wapatao 38 na wengine 18 kujeruhiwa.
Magaidi hao wamedai kuuwa wanajeshi wa nchi hiyo wapatao 61 na kuteka magari ya kijeshi yapatao 15 katika mashambulio hiyo.
Muhammad Abdullah (ambaye ni Rais wa nchi hiyo) amesema kufuatia shambulio la magaidi ho dhidi majesh ya nchi hyo kuwa: majeshi ya taifa hilo yatalipiza mauaji hayo na kukisambaratisha kikundi hicho cha kigaidi nchini humo.
Aidha Rais wa nchi hiyo amekemea vikali mauaji hayo nakuyasifu kuwa ni mauaji ya kinyama na akatoa kauli yakuwa kikundi cha kigaidi cha Al-Shaba atakabiliana nacho vikali na kukifuatilia kikundi hicho popote kitakapo jificha, huku akisistiza kuto vihurumia vikundi hivyo kwa nji yoyote.
Inasemekana kuwa kikundi cha kigaidi cha Al-Shabab kimeasisiwa mwaka 2007 kwaajili ya kuitoa serikali ya Somalia, manamo mwaka 2011 ilitekwa sehemu ya mkoa na kambi walikuwa wakiimiliki katika mji wa Afgooye nchini humo.
Mnamo mwaka 2012 kikundi hicho kiliungana na kikundi cha kigaidi cha Alkaida, ambapo kilfanikiwa kuyateka maeneo ya kusini mwa Somalia, ama baada ya kufika mwaka 2015 kilishindwa kuendelea kuyamiliki maeneo hayo na mpaka sasa wapo katika sehemu ya baadhi ya vijiji vya nchi hiyo.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky