Mpaka mwaka 2040 dini ya Uislamu itakuwa ya pili baada ya Ukristo nchini Marekani

Mpaka mwaka 2040 dini ya Uislamu itakuwa ya pili baada ya Ukristo nchini Marekani

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na taasisi ya uhakiki ya Pew iliopo nchini Marekani, imetoa ripoti inayoonyesha kuwa idadi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu nchini Marekani mpaka mwaka 2040 itakuwa dini ya pili kwakuwa na wafuasi wenge nchini humo

Shirika la habari AhlulaBayt (a.s) ABNA: taasisi ya uhakiki ya Pew ya kimarekani imetangaza tija ya uchungu wake iliofanya kuhusu idadi ya waislamu katika taifa hilo, na kusisitiza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2040, idadi ya Waislamu itakuwa na nafasi ya pili baada ya Ukristo nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti iliosambazwa na taasisi hiyo ni kwamba idadi ya Waislamu hivi sasa nchini humo katika mwaka 2017 ni milioni 3.45, ambapo kunaonekana na ongezeko la asilimia 1.1 kwa idadi nzima ya waislamu wa nchi hiyo.
Ripoti ya uhakiki wa taasisi hiyo imeeleza kuwa, jamii ya Waislamu imeonekana inapanuka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na jamii ya Kiyahudi katika nchi hiyo, taasisi ya uhakiki ya Pew inaamini kuwa, kukuwa kwa jamii ya kiislamu kutaendelea ambapa ifikapo mwaka 2050 idadi ya Waislamu itakuwa milioni 8.1, huku taasisi hiyo ikibainisha kuwa kwa hali yaki, jamii ya waislamu wa Marekani kila mwaka huongozeka watu laki moja.
mwesho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky