Mwanamke Mwislamu Marekani adungwa kisu na mtu aliyekuwa akiutusi Uislamu

Mwanamke Mwislamu Marekani adungwa kisu na mtu aliyekuwa akiutusi Uislamu

Serikali ya Jimbo la Texas nchini Marekani imetangaza zawadi ya $5000 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa mtu ambaye alimdunga kisu mwanamke Mwislamu katika mji wa Houston.

Kwa mujibu wa Tawi la Houston la Baraza la Uhusiano wa Kiislamu Marekani, CAIR, mwanamke Mwislamu mwenye umri wa miaka 25, ambaye ni mzunngu na kwa kawaida huvaa vazi la Hijabu aliropoti kuwa, siku ya Alhamisi asubuhi alikuwa akiendesha gari kutoka sehemu anayofanya kazi
kama muuguzi wakati gari lilipomgonga kwa makusudi. Wakati alipotoka kuangalia uharibifu wa gari lake, aliyemgonga alitoka ndani ya gari lake na kumkejeli na kumtusi huku akitoa matamshi yenye chuki dhidi ya Uislamu.
Anasema anaamini uhasama huo ulitokana na kuwa alikuwa amevaa Hijabu. Anaongeza kuwa alipojairbu kurejea katiika gari lake ili kuepuka shari ya mtu huyo, ndipo alipodungwa kisu mkononi na begani. Anasema mpitanjia ndiye aliyemzuia mwanaume huyo kuendelea na hujuma yake hiyo.

Mwanamke huyo Mwislamu alirejea katika hospitali anapofanya kazi na kupata matibabu ya dharura. Mwenye kutekeleza hujuma hiyo anasemekana kuwa mwanamume mzungu alieykuwa na umri wa kati ya miaka 20-25.

Mkurugenzi wa CAIR Tawi la Houston Mustafa Carrol ametoa wito kwa yeyote mwenye habari kuhusu mtu huyo ambaye ametajwa kuwa hatari awasiliane na maafisa wa usalama.
............
300


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky