Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amuidhinisha Rouhani kuwa Rais wa Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amuidhinisha Rouhani kuwa Rais wa Iran

TEHRAN (IQNA)-Sherehe ya kuidhinisha kura za wananchi kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu zimefanyika leo hapa Tehran kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kumuidhinisha Hassan Rouhani kuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika dikrii aliyotoa katika sherehe hiyo iliyofanyika katika  Husseiniya ya Imam Khomeini MA, ameutaja uchaguzi uliohudhuriwa na wananchi wengi na kupata kura nyingi shakhsiya aliyechaguliwa kuwa ni ishara ya kuimarika upande wa Jamhuri wa utawala wa Kiislamu wa Iran na amesisitiza udharura wa kutekelezwa mpango wa uchumi wa ngangari.

Ayatullah Khamenei amemtaka Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuelekeza jitihada zake katika kutekeleza uadilifu, kuwatetea wale wote walionyongeshwa na maskini, kutekeleza sheria za Kiislamu, kuimarisha umoja na heshima ya taifa na kutilia maanani uwezo mkubwa wa nchi na kuwa wazi katika kutukuza thamani na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Halikadhalika katika sherehe hiyo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran ametoa ripoti kuhusu namna uchaguzi wa 12 wa Rais ulivyofanyika hapa nchini.

Kwa mujibu wa kifungu cha 110 cha Katiba ya Iran, miongoni mwa majukumu na mamlaka ya Kiongozi Muadhamu ni kusaini na kupasisha dikrii ya Rais wa nchi baada ya kuchaguliwa na wananchi. Kipindi cha urais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miaka minne na Rais huanza kutumikia wadhifa wake baada ya tarehe ya kuidhinishwa hati za utambulisho wake na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Hassan Rouhani kwa mara nyingine tena alichaguliwa kuwa Rais wa Iran katika duru ya 12 ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uliofanyika Mei 19 mwaka huu kwa kupata kura zaidi ya milioni 23 au tarkibani asilimia 57 ya kura zilizopigwa.
...........
300


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Quds cartoon 2018
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky