Kongamano la Kiislamu Misri lataka waungaji mkono ugaidi wachukuliwe hatua

Kongamano la Kiislamu Misri lataka waungaji mkono ugaidi wachukuliwe hatua

Kongamano la kimataifa la Kiislamu la kupambana ugaidi limefanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo ambapo wanazuoni walioshiriki wametaka nchi zote duniani zichukue hatua kali dhidi ay waungaji mkono ugaidi.

Hayo yamebainika katika Kongamano la 28 la Kimataifa la Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu lilifanyika Jumatatu na Jumanne mjini Cairo ambapo wanazuoni, wanafikra na wataalamu kutoka nchi 50 walishiriki ambapo mada kuu ilikuwa ni: "Sekta ya Ugaidi na Njia za Kukabiliana Nayo."

Taarifa ya mwisho ya kongamano hilo imesisitiza haja ya serikali kuchukua hatua za kukabiliana na ugaidi na pia kuweza kuvuka vizingiti katika jitihada hiyo.

Halikadhalika washiriki wamesema jamii zina jukumu ya kutangaza msimamo imara wa kupinga kikamilifu ugaidi na magaidi. Aidha taarifa hiyo imetaka kuchukuliwa hatua za kusitisha misaada ya kifedha na misaada mingine yote ambayo hufikia makundi ya kigaidi. Washiriki katika mkutano huo pia wametilia mkazo umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii kuelimisha umma kuhusu njia za kukabiliana na ugaidi.
..............
300


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky