Umoja wa Ulaya: watakao ewekea kikwazo Iran naye tutamuwekea vikwazo

Umoja wa Ulaya: watakao ewekea kikwazo Iran naye tutamuwekea vikwazo

Mshauri wa kiongozi wa siasa za mambo ya nje katika umoja wa Ulaya amesema: mashirika ya Ulaya ambayo yatafuata na kutekeleza vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran, Umoja wa Ulaya utamuwekea kikwazo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: msaidizi wa “Fedrika Mughirini” ambaye ni msimamizi wa siasa za mambo ya nje katika umoja wa Ulaya amesema kuwa mashirika yote ya Ulaya ambayo yatafuata na kutekeleza vikwazo vya marekani dhidi ya Iran, Umoja wa  Ulaya yataweka vikwazo dhidi ya mashirika hayo.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa maamuzi hayo ni kwaajili ya kuhifadhi mashirika ya Ulaya yasifuate vikwazo vya upande mmoja vinavyowekwa na Marekani dhidi ya Iran, kadhalika kutuma ujumbe kwa Iran kuwapa uhakika kuwa wako katika juhudi za kuendeleza makubaliano ya mpango wa nyuklia.
Kwa upande mwingine amesema: vikwazo vitakavyo wekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya mashirika hayo ni vikwazo mbalimbali ikiwemo kuyafunga mashirika hayo, pamoja ya kuwa mpaka sasa hatujaainisha masharti na jinsi tutakavyo yafungia mashirika hayo.
Aidha mkuu wa masuala ya siasa za nje katika umoja wa Ulaya amesema mbele ya waandishi wa Habari kuwa, umoja huo unafanya juhudi za  makusudi za kuifanya ibaki katika makubaliano ya mpango wa Nyuklia ambao Marekani ilishakuwa imejitoa.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky