Kijana afungwa miaka 4 jela kwa kosa la kueneza fikira za kigaidi nchini Ufaransa

Kijana afungwa miaka 4 jela kwa kosa la kueneza fikira za kigaidi nchini Ufaransa

Mtu mmoja nchini Ufaransa ahukumiwa kufungwa miaka 4 jela kwakosa la kusambaza bendera ya kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mitandao ya kijamii nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: moja katika mahakama ziliopo katika mji wa Nimes kusini mwa Ufaransa, imemuhukumu mtu mmoja miaka 4 jela kwa kosa la kupeperusha na kusambaza bendera ya kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mitandao ya kijamii nchini Ufaransa.
Mtu huyo aliyekuwa na umri wa miaka 30 hapo awali alifungwa miaka mitano jela kwa kosa la kushiriki katika kikundi fulani kilichokuwa na fungamano na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Aidha awali alihumiwa kufungwa miezi sita jela kufuatia kosa hilo, ama baada ya kutolewa hukumu hiyo mahaka ilidai kuwa muda aliohukumiwa ni mchache ndipo ikaongezwa na kufikia miaka minne kutumikia kifungo hicho.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky