Magaidi 14 wa kikundi cha PKK wauwawa kwa kushambuliwa na majeshi ya Uturuki

 Magaidi 14 wa kikundi cha PKK wauwawa kwa kushambuliwa na majeshi ya Uturuki

Magaidi 14 wa kikundi cha kigaidi cha PKK cha Wakurdi nchini Uturuki wapoteza maisha kufuatia shambulio liliofanywa na majeshi ya Uturuki nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: makao makuu ya majeshi ya Uturuki yametangaza kuwa, ndege za nchi hiyo zimefanya mashambulizi katika sehemu ya mashariki mwa Uturuki na kaskazini mwa Iraq na kuangamiza 14 wa magaidi wa PKK katika maeneo hayo.
Mashambulizi ya majeshi ya Uturuki katika maeneo ya kaskazini ambayo yalianza miezi minne iliopita, katika wiki za hivi mwishoni ilifanikiwa kuanisha maeneo maalumu katika miinuko ya Qandil katika mipaka ya Iraq kwaajili ya kuwasambaratisha magaidi waliopo katika miinuko hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti za majeshi ya Uturuki katika shambulio liliofanyika mwishoni yaliofanywa na ndege zake katika miinuko hiyo, limefanikiwa kuuwa wmagaidi 14 wa kikundi cha PKK cha Wakurdi wa sehemu hiyo.
Kikundi cha kigaidi cha PKK mpaka kina miaka zaidi ya 30 kinafanya mashambuizi dhidi ya serikali ya Uturuki, ambapo kikundi hicho kilitangazwa kuwa ni cha kigaidi na Uturuki kisha umoja wa Ulaya na mwisho serikali ya Marekani nayo ilitangaza kuwa kikundi hicho kuwa ni chakigaidi.
Kikundi hicho kwa sasa katika maeneo ya miinuko na milima ya mashariki na kusini mwa mashariki mwa Uturuki, vilevile miinuko ya kaskazini mwa Iraq na kufanya matukio ya kigaidi katika sehemu mbalimbali.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky