Majeshi ya anga ya Urusi yasambaratisha sehemu 1000 za vikundi vya kigaidi nchi Syria

Majeshi ya anga ya Urusi yasambaratisha sehemu 1000 za vikundi vya kigaidi nchi Syria

Majeshi ya anga ya Urusi katika kipindi cha wiki moja yarusha ndege za kivita 440 katika anga la Syria ambapo ndege hizo zimeshambulia sehemu elfu za magaidi wa nchi hiyo na kuzisambaratisha

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya ulinzi na uslama ya Urusi imetangaza kuwa: majeshi ya anga ya nchi hiyo kwa muda wiki moja yamerusha ndege za kivita 440 katika anga la Syria na kushambulia zaidi ya maeneo ya 1000 ya vikundi vya kigaidi viliopo nchini humo na kuzisambaratisha.
Wizara hiyo pia imetangaza kuwa ndege zake zisikuwa na Rubani kwa wiki moja zimerushwa zaidi ya mara miamoja kwaajili ya kuchukua ripoti muhimu za magaidi hao ikiwemo makazi na maficho muhimu wanayojificha magaidi hao nchini Syria.
Aidha majeshi maalumu ya Urusi kwa wiki mija yamefanikiwa kuzikomboa zaidi ya hekta 140 kutoka mikononi mwa magaidi huku wakifanikiwa kutegua mabomu 700 katika sehemu hiyo kwa muda wiki moja.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky