Mogherini: asisitiza kuwa umoja wa Ulaya utashikamana na muafaka wa nyuklia wa Iran

Mogherini: asisitiza kuwa umoja wa Ulaya utashikamana na muafaka wa nyuklia wa Iran

Kiongozi wa masuala ya siasa za nje katika umoja wa Ulaya amesisitiza kushikamana kwa umoja wa Ulaya kunako makubaliano ya mbango wa nyuklia wa Iran, huku akiayataka mataifa mengine yalioshiriki makubaliano hayo, kuheshimu makubaliano ya mpango huo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA:Federica Mogherini kiongozi wa siasa za nje katika umoja wa Ulaya, aliyasema hayo baada ya kutoka katika kikao na mawaziri wa mambo ya nje wa Iran, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa na kutangaza kuwa: Umoja wa Ulaya unashikamana na makubaliano kwakuwa ni jambo muhimu katika kulinda amani na usalama na tunazitaka kila pande kushikamana na makubaliano hayo na kuyatekeleza kikamilifu makubaliano hayo.
Aidha ameongeza kusema kuwa: suala utengenezaji wa makombora ya masafa marefu na na mizozo inayotokea katika ukanda wa mashariki ya kati hayakuwepo katika makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran, hivyo linapaswa kuzungumziwa nje ya mpango wa nyuklia.
Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa: makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran unafaida kubwa sana na utasaidia kuleta amani na usalama wa kimataifa na kupunguza mashindano ya kutengeza silaha za maangamizi ulimwenguni.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky