Msikiti wavunjiwa heshima Ujerumani

Msikiti wavunjiwa heshima Ujerumani

Watu wenye chuki dhidi ya Uislamu wameuvunjia heshima msikiti ambao bado unajengwa katika mji wa Frankfurt, Ujerumani Jumanne.

Taarifa zinasema watu wasiojulikana wameweka kichwa cha nguruwe katika eneo la msikiti unaojengwa na Jumuiya ya Waislamu wa Uturuki ijulikanayo kama Ditib. Kumekuwepo na upinzani mkali wa ujenzi wa mji huo. Taarifa zinasema wakaazi wa mji huo wameandamana mara kadhaa kupinga ujenzi wa msikiti huo wakitaka leseni yake ibatilishwe.

Jumuiya ya Waislamu wa Uturuki inafadhili misikiti 900 kote Ujerumani, nchi ambayo ina Waislamu milioni tatu wenye asili ya Uturuki.

Katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Waislamu huku chama cha AfD kinachopinga Waislamu kikipata asilimia 13 ya kura katika uchaguzi wa mwezi jana nchini humo.
...............
300


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Arba'een
Mourining of Imam Hossein
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky