Ongezeko la hujuma dhidi ya misikiti nchini Sweden

Ongezeko la hujuma dhidi ya misikiti nchini Sweden

Misikiti nchini Sweden ilishambuliwa mara 38 mwaka 2017, ikiwa ni ongezeko la mara 10 ya vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Uislamu.

Kwa mujibu wa  ripoti ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Uppsala nchini humo, kumeshuhudiwa ongezeko kubwa sana la hujuma dhidi ya misikiti katika nchi hiyo ya eneo la Skandinavia barani Ulaya.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Seden Morgon Johansson amelitaja ongezeko hilo kuwa lenye mbaya mno. Ameongeza kuwa, kuibuka makundi ya mrengo wa kulia ya utaifa wenye misimamo mikali kote Ulaya ni jambo ambalo limewatia katika matatizo makubwa wahajiri, hasa Waislamu, na jambo hilo limehatarisha mno usalama na uhuru wao.

Johansson amesema serikali ya Sweden inapanga kuunda kikosi maalumu cha polisi kuilinda misikiti sambamba na kuongeza idadi ya kamera za usalama.

Naye Max Stockman wa Tume ya Serikali ya Sweden ya Kuunga Mkono Dini za Waliowachache amesema ongezeko la hujuma dhidi ya misikiti ni tishio kubwa kwa uhuru wa kuabudu nchini humo.

"Kila mtu anapaswa kuishi kwa usalama katika dini yake," ameiambia televisheni ya kitaifa, SVT.

Kufuatia uchaguzi mkuu wa Sweden uliofanyika Septemba 9, ilibainika kuwa chama cha mrengo wa kulia na kinachopinga wahajiri cha Sweden Democrats, kilipata uungaji mkono asilimia 20.

Kati ya watu milioni 10 nchini Sweden, karibu milioni 1.4 walizaliwa nje ya nchi hiyo.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la hujuma dhidi ya misikiti kote barani Ulaya katika miaka ya hivi karibuni kufuatia mafanikio vya vyama vya utaifa wa kufurutu ada na vyenye chuki dhidi ya Uislamu.
...............
300


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky