Uturuki: kamwe hatutafuata vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran

Uturuki: kamwe hatutafuata vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema: vikwazo vya Marekani vilivyo wekwa dhidi ya Iran kamwe hatutavitekeleza na kuvifuata

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki na kusisitiza kuwa kamwe Uturuki haitatekeleza na kufuata vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
“Mavlut Cavusoglu” waziri wa mambo ya nje wa Uturuki alibainisha alipokuwa ameonana na Mahmud Waidhiy” msimamizi wa msafara maalumu wa Iran ulitumwa kwenda nchini Uturuki walipokuwa wakijadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la utawala wa Marekani kutoka katika makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran.
Kwa upande mwingine Waidhi amesema kuwa mataifa ya Ulaya na umoja wao kwa ujumla inaonekana wako kao katika juhudi ya kuhifadhi makubaliano ya mpango wa Nyuklia wa Iran, alkadhalika kutoa maoni yao kwa serikali ya Iran kunako masuala ya kibiashara, uchumi na mafuta.
Waidhiy ambaye alikwenda nchini Uturuki kufikisha ujumbe wa rais wa Iran kwa rais wa jamhuri ya Uturuki, pia alizungumzia masuala ya fungamano ya mataifa hayo mawili na jinsi ya zitakuza uhusiano wa nchi hizo.
Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Uturuki baada ya kuonana na Waidhiy alisambaza ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter alitangaza kuwa ameonana na Mahmud Waidhiy mkuu wa ofisi ya Rais wa Iran na tumezungumzia mambo mbalimbali ya mataifa hayo mawili.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky