Vyombo vya habari Uingereza vina mtazamo hasi kuhusu Waislamu

Vyombo vya habari Uingereza vina mtazamo hasi kuhusu Waislamu

Baadhi ya vyombo vya habari vya Uingereza vina mtazamo hasi kuhusu Uislamu na Waislamu na hali hivi sasa ni mbaya zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2011, amesema mjumbe Muislamu katika Bunge la Malodi la Uingereza Bi. Sayeeda Hussain Warsi

Akitoa ushahidi Jumanne katika  Kamati ya Mambo ya Ndani ya  Bunge au Baraza la Wawakilishi (la Commons ) kuhusu 'hujuma za chuki na taathira zake mbaya', Bi. Warsi amesema Waislamu Waingereza mara kwa mara hulengwa katika baadhi ya magazeti ya nchi hiyo.  "Ninaweza kuzungumza kwa masaa kadhaa kuhusu namna magazeti yanayoonyesha taswira hasi kuhusu Waislamu," amesema.

Warsi amesema ni jambo la kawaida sasa kuona wananchi wakitiwa sumu kupitia Makala zinazolenga kuonyesha taswira mbaya ya Waislamu.

Naye Chris Frost, mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Waandishi Habari Uingereza anasema tatizo hilo la kuwalenga na kuwabagua Waislamu sasa ni kubwa. Amesema ni jambo la kushangaza kuona namna baadhi ya wahariri huamuru maripota kuandika vibaya kuhusu Waislamu. "Moja ya njia ya kuuza gazeti kwa wingi ni kuwafanya watu waamini kuwa kuna hatari. Sasa kwa sababu ya ISIS (Daesh), Waislamu wanalengwa," amesema.

Frost amesema karibu asilimia 64 ya watu wa Uingereza hujifunza kuhusu Uislamu na Waislamu katika magazeti na huamini kilichoandikwa bila ya kutaka kufanya utafiti au kupata maelezo kutoka sehemu nyingine.

Bi.Warsi ameifahamisha kamati hiyo kuwa hivi sasa wasichana Waislamu wanaovaa Hijabu na Waislamu wengine wanaoweza kuutambuliwa haraka, wakiwa katika vituo vya reli zinazopita chini ya ardhi (tube) hufadhilisha kusimama katika safu za nyuma kwa kuhofia kusukumwa katika reli na watu wenye chuki.

Bi.Warsi ametoa wito kwa waziri mkuu wa Uingereza na kiongozi wa upinzani kutoa hotuba zinazooonyesha namna Waislamu waliovyota mchango mkubwa nchini humo.
............
300


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky