Kuanguka kwa ndege ya Misri kumetokana na mripuko wa bomu

  • Habari NO : 755903
  • Rejea : ABNA
Brief

Vyombo vya habari vya Marekani vimedai kuwa kuanguka kwa ndege ya Misri kumesababishwa na mripuko wa bomu liliokuwa limewekwa ndani mwa ndege hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: baadhi ya vyombo vya habari vya  Marekani vikinukuu kutoka kwa viongozi wa nchi hiyo vimetangaza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa katika ndege hiyo kulikuwa na bomu ndani mwake ambapo baada ya kuripuka ndiko kukasababisha kuanguka kwa ndege hiyo.
Ndege moja ya shirika la ndege la Misri alianguka asubuhi ya alhamisi iliopita katika bahari ya Mediterranea, ambapo ndege hiyo ilikuwa inatoka Ufaransa kwenda Cairo nchini Misri na ndani ya ndege hiyo kulikuwa na abiria 66 ambapo wote wameriki dunia, huku magaidi wa Daeshi wamedai kuhusika na tukio hilo, huku watishia kushadidisha mashambulizi ya kigaidi katika bara la Ulaya na Marekani hasa katika kipindi cha legi za michezo ya Ufaransa ambayo inatarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Miezi kadhaa iliopita ndege ya abiria ya Urusi nayo alianguka katika jangwa la Sinai nchini Misri ambapo sababu ya kuanguka ndege hiyo ni kuripuka bomu liliokuwa limewekwa ndani ya ndege hiyo na magaidi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
mwisho wa Habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky