Kamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Libya aangamia

  • Habari NO : 759346
  • Rejea : ABNA
Brief

Mmoja kati ya makamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Libya amiangamia katika mji wa Sirte nchini Libya

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mmoja kati ya makamanda wa kikundi cha kigaidi cha Daesh Libya anaye fahamika kwa jina la “Hamid Al-zalitini” ameangamia katika mashambulizi makali yaliotokea baina ya majeshi ya serikali ya Libya na kikundi cha kigaidi cha Daesh yaliofanywa pembezoni mwa mji wa Sirte nchini humo.
Katika mashambulizi hayo makali magaidi wengine wa kikundi cha Daesh pia wameangamia ambapo habari za kuangamia kwao zimethibitishwa rasmi na viongozi wa kikundi hicho cha kigaidi.
Majeshi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh yaliopo katika mji wa Sirte yako tayari muda wowote kuanza mapigano kutokana na mapigano makali yalio tokea hivi karibuni baina ya kikundi hicho cha kigaidi na majeshi ya serikali ya Libya pembezoni mwa mji wa Sirte na maingilio ya mji huo.
Harakati za kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Libya zaidi ya mwaka mmoja toka zianze harakati zake nchini humo, na mji wa Sirte ndio umekuwa makao makuu ya kikundi hicho nchini Libya.
mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky