Muhammad Mursiy ahukumiwa kifungo cha maisha

  • Habari NO : 761093
  • Rejea : ABNA
Brief

Muhammad Mursiy Rais aliopita wa Misri amehukumiwa kifungo cha maisha jela kufuatia kesi ya kuifanyia ujasusi kwaajili ya Qatar

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mahakama kuu ya makosa ya jinai mjini Cairo imemuhukumu Muhammad Mursiy rais wa zamani wa Misri kifungo cha maisha kwa tuhuma ya kufanya ujasusi kwaajili ya Qatar ambapo kwa mara ya kwanza alihukumiwa miaka 15 jela na kwa mara nyingine amehukumiwa kifungo cha milele kwa rais huyo.
Ukiacha Muhammad Mursiy kuna waliohukumiwa wengine ikiwemo Ahmad Abdulatiy na Amin Swairafiy ambao wamehukumiwa kifungo cha maisha nchini humo huku wengine sita wakihukumiwa kunyongwa na mahakama hiyo.
Uhakiki wa Mahakama kuu ya nchi hiyo kuhusiana faili la “ujasusi kwaajili ya Qatar” umeonyesha kuwa Muhammad Mursiy na watuhumiwa wengine kadhaa kwamba wametuhumiwa kuchukua ripoti zilizotoka kwa kiongozi wa vita, majeshi, vyombo vya usalama wa taifa, wizara ya mambo ya ndani  ambapo katika hizo kuna nyaraka za siri za serikali hiyo, nyaraka ambazo zinaonyesha sehemu za majeshi na siasa za uendeshaji wa nchi, Watuhumiwa hao walikusudia kwamba nyaraka hizo kuzikabidhi kwa serikali ya Qatar na televisheni ya Aljazirah    
mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky