Hijja ni jambo la Ibada hivyo mahujaji hawapaswi kujuhusisha na mambo ya kisiasa

  • Habari NO : 773273
  • Rejea : ABNA
Brief

wizara Hajji nchini Misri: Hijja ni jambo la kiibada na haliko katika masuala ya kisiasa, hivyo ni vyema kwa mahujaji wote kuacha kujihusisha na masuala ya siasa wanapokuwa katika ibada ya Hijja na kuzumgumzia mambo ya kisiasa na kuacha misingi ya ibada hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya Hijja na mambo ya waqfu nchini Misri katika kauli yake iliochapishwa katika vyombo vya habari vya nchi hiyo, imewataka masheikh na wanaongozaji wa mahujaji wa nchi hiyo kuwa ”wanapaswa kutekeleza nyadhifa zao katika kuwachunga na kuwafahamisha mambo ya kisheria mahujaji wa nyumba ya mwenyezi Mungu, ili waweze kutekeleza matendo ya Hijja kama inavtotakiwa, na hawapaswi kujiingiza katika mijadala na masuala ya kisiasa”.
Katika kauli hiyo imeelezwa kwama “Hija ni suala la kiibada na si suala la kisiasa, na mahujaji hawapaswi kujiingiza katika mambo ya kisiasa pale wanapokuwa katika Hijja, na kuacha matendo ya ibada hiyo na kujihusisha na mambo yasiowahusu”
Wizara hiyo imetangaza jambo hilo katika hali ambayo mashiko ya kislamu yanaashiria kuwa Hijja ni jambo la ibada pia ni jambo la kisiasa “kwani mtukufu mtume Muhammad (a.s.w.w) iliitumia Hijja katika kufikisha mambo ya kisiasa suala ambalo lilipelekea watu wa Madina kujiunga na dini ya Uislamu na hatimaye kupatikana serikali ya Kiislamu ya bwana mtume katika mji wa Madina.
Katika mjumuiko wa kibada na kisiasa wa Hijja waislamu wote ulimwenguni hukusanyika na kufahamishana mambo mbalimbali yanayojiri katika maeneo wanaoishi waislamu na changamoto zinazowakumba kutoka kwa maadui wa Uislamu hatimaye kuchukua hatua na maamuzi ya pamoja kama waislamu.
Maadui wa uislamu daima wamekuwa wakifanya juhudi za kulifanya suala la Hijja kuwa limejifunga na upande wa kiibada pekee na halinafungamano lolote na mambo ya kisiasa, kwani wanafahamu kwa wazi kuwa suala kama litafanywa katika hali ya dhahiri kama wanavyotaka hakuana madhara yeyote yatakayowapata, ama kinyume chake haitakuwa kwa masilahi yao.   
mwisho wa Habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky