Marekani

Brigedia Salami: Madai ya Marekani dhidi ya Iran ni hadaa

  • Habari NO : 271590
Abna inatuarifu kuwa:Kamanda wa ngazi za juu wa Kikosi cha Kulinda Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Brigedia Hussein Salami amesema madai ya Marekani kwamba Iran ilihusika na njama ya kumuua balozi wa Saudi Arabia mjini Washington ni hadaa na hayaingii akilini.
Abna inaendelea kutuarifu kuwa:Brigedia Salami amesema kuwa, madai hayo ya Marekani yasiyokuwa na mashiko wala msingi ni moja  kati ya  njama za dola hilo la kibeberu za kujaribu kuichanganya jamii ya kimataifa mkabala na kuelekea kufeli kwa mfumo wake wa kibepari. Matamshi ya afisa huyo wa ngazi za juu wa jeshi la Iran yanaenda sambamba na tamko la Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliyesema kuwa, tuhuma hizo za Marekani ni mchezo uliofeli na hata Wasaudia wenyewe wanaelewa vyema mchezo huo na taathira zake. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa uhusiano wa Iran na nchi za Ghuba ya Uajemi ni mzuri.Serikali Tehran imesisitiza kwamba, uhusiano wake na Serikali ya Riyadh ni mzuri licha ya hitilafu za kimtazamo ziliopo kati ya pande hizo mbili kuhusu matukio ya eneo la Mashariki ya Kati.  


بی کفایتی آل سعود
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky