Marekani

Iran yakanusha madai ya Marekani kuhusu njama za kumuua balozi wa Saudia

  • Habari NO : 271438
Abna inatuarifu kuwa:Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekanusha madai ya uwongo kwamba kumekuweko na mpango wa kutaka kumuua balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani na kueleza kuwa madai hayo yanayoihusisha na Iran na tuhuma hizo yako mbali na uhakika.

Ramin Mehmanparast amelaani oparesheni yoyote ya kigaidi katika radiamali yake kwa madai yasiyo na msingi yaliyotolewa na viongozi wa Marekani kwamba Iran imeshiriki katika mpango wa kutaka kutekeleza oparesheni ya kigaidi huko Marekani. Ramin Mehmanparast amesema miamala mibovu kama hiyo iliyojengeka juu ya siasa za kiadui na zilizopitwa na wakati za Marekani na Uzayuni inatekelezwa kwa malengo maalumu na maadui wa Uislamu na wa eneo hili. Ameongeza kuwa wapangaji wa njama hizo hawana lengo jingine ghairi ya kuzusha hitilafu na kusaidia kuuondoa utawala wa Kizayuni kwenye hali ya kutengwa.


بی کفایتی آل سعود
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky