Mripuko mkubwa watokea katika mji wa Homs nchini Syria

  • Habari NO : 810688
  • Rejea : ABNA
Brief

Bomu la kigaidi laripuka katika mji wa Homs nchini Syria lasababisha mauaji ya wananchi watatu nchini humo na wengine kujeruhiwa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari nchini humo vyantangaza kutoke mripuko mkubwa wa kigaidi nchini Syria.
Siku ya Alhamisi vikundi vya kigaidi nchini Syria vilitegesha bomu katika midani iliopo sehemu ya “Al-zahra” katika mji wa Homs na hatimaye kuripuka, ambapo watu watatu miungoni mwa wananchi wa Syria wamepoteza maisha kufuatia mripuko huo na wengine wawilui kujeruhiwa.
Mpaka sasa hakuna kikundi chochote cha kigaidi kilicho tangaza kuhusika na tukio hilo, ama kunaishara kubwa inayonyesha kuwa tukio hilo limefanywa na kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Kabla ya mripuko huo kulitokea miripuko kadhaa ya kigaidi katika mji wa Homs sehemu ya Zahra, amapo kufuatia miripuko hiyo mamia ya wananchi wasio na hatia walipoteza maisha.
Mji wa Homs uko chini ya majeshi ya Syria, ama vikundi vya kigaidi kama vile Daesh vipo sehemu ya Hume ya kaskazini mwa mashariki ya mji huo.
Majeshi ya serikali ya Syria katika mashambuli yake hivi mwishoni yameweza kusonga mpele kwa kiasi kikubwa katika sehemu Hume ya mashariki ya mji wa Homs katika kukabiliana na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.   
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky