Sehemu ya “Palestina” yakombolewa katika mji wa Musol

  • Habari NO : 804074
  • Rejea : ABNA
Brief

Majeshi ya Iraq yamefanikiwa kuikomboa sehemu Inayoitwa Palestina iliopo katika mji wa Musol kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, hatimaye kuwa mikononi mwa majeshi ya Iraq kikamilifu

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Iraq yamefikia ushindi mwingine mpya dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo majeshi hayo siku ya Jumatatu yameweza kuikomboa sehemu inayoitwa Palestina kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Hayo yamesemwa na kamanda wa mashambulizi ya Musol “Abdulamir Rashidi Yarallah” kuwa wamefanikiwa kuikomboa sehemu ya “Palestina” katika fukwe ya kushoto mwa mji wa mji huo.
Kwa mujibu wa maelezo ya kamanda huyo ni kwamba katika mashambulio ya kuikomboa sehemu hiyo, kikundi cha kigaidi cha Daesh kimepata maafa makubwa kufuatia shambulio hilo.
Aidha majeshi hayo pia yamefanikiwa kuliteka daraja la nne katika mto wa Tigris mashariki mwa mji wa Musol.
Majeshi ya Iraq toka miezi mitatu iliopita walianza utangulizi wa mashambulizi ya kuukomboa mji wa Musol, ambapo mpaka saa wamefanikiwa kuyakomboa maneo mengi ya mji huo kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh kimetumia njia nyingi kwaajili ya kuzoofisha hatua ya ukomboaji wa mji Musol, ikiwemo kutega magari yaliokuwa na mabumu na kufanya miripuko ya kigaidi katika sehemu mbalimbali nchini humo, ama mpaka sasa hawajaweza kusitisha harakati za kuukomboa mji huo.
mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky