Kundi la Hamas lachagua kiongozi mpya Gaza

  • Habari NO : 811530
  • Rejea : abna.ir
Brief

Chama cha ukombozi wa wapalestina cha Hamas leo kimemchagua mwanachama wake mwenye msimamo mkali wa kitengo cha kijeshi Yahya Sinwar kuwa mkuu mpya wa Ukanda wa Gaza.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Chama cha ukombozi wa wapalestina cha Hamas leo kimemchagua mwanachama wake mwenye msimamo mkali wa kitengo cha kijeshi Yahya Sinwar kuwa mkuu mpya wa Ukanda wa Gaza. Maafisa wa Hamas wamesema Sinwar ataiongoza ofisi ya masuala ya siasa ya kundi hilo na atamrithi Ismail Haniya, anayeonekana na wachambuzi wengi kuwa mtu atakayechukua nafasi ya kiongozi wa Hamas aliye uhamishoni Khaled Meshaal. Septemba 2015 Sinwar aliwekwa katika orodha ya Marekani ya watu wanaojihusisha na ugaidi pamoja na wanachama wengine wawili wa kitengo cha kijeshi cha Hamas, Ezzedine al Qassam Brigades. Marekani inamtuhumu kwa kuendelea kupigania utekaji nyara wa wanajeshi wa Israel kama njia ya kulazimisha mazungumzo kwa niaba ya wafungwa wa kipalestina.

Israel kwa msaada wa Uingereza, Ufaransa na Marekani ilidhulumu sehemu kubwa ya ardhi ya wapalestina, wananchi wa Palestina wanaopigana kurudisha ardhi zao wanauwa na wengine wanaitwa magaidi.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky