Wanajeshi 6 wa jeshi la Uturuki wauwawa kufuatia mapambano na kikundi cha kigaidi cha PKK

  • Habari NO : 781648
  • Rejea : ABNA
Brief

Watu sita kutoka katika jeshi la Uturuki wameuwawa katika kufuatia mapambano yaliotokea kati ya kikundi cha kigaidi cha kigaidi cha PKK kusini mwa mashariki ya Uturuki

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Uturuki yatangaza habari ya kuuwawa kwa wanajeshi wake kadhaa kufuatia mapambano yaliotokea kati ya jeshi hilo na kikundi cha kigaidi cha PKK.
Katika mashambulio hayo imeripotiwa kuuwawa wanajeshi 6 wa jeshi la nchi hiyo katika mashambulizi hayo kati yake na kikundi cha kigaidi cha PKK kusini mwa mashariki mwa Uturuki.
Aidha mapambano hayo kati ya wanajeshi wa Uturuki na wanamgambo wa kikundi cha kigaidi cha PKK yametokea katika kituo cha ukaguzi wa kijeshi katika sehemu ambayo iko karibu na jela iliopo katika mkoa wa Şırnak nchini Uturuki.
Kuhusu maafa waliopata kikundi cha kigaidi cha PKK katika mapambano hayo na jeshi la Uturuki mpaka sasa bado haijafahamika.
Kwa muda wa wiki kadhaa ziliopita makumi ya majeshi ya Polisi na jeshi la nchi hiyo waliuwawa katika mapigano na kikundi cha kigaidi cha PKK katika maeneo wanayoishi Wakurdi nchini humo.
Kikundi cha kigaidi cha PKK kilitangaza kuanza mapambano ya silaha na serikali ya Uturuki toka miaka takriban 30 iliopita, ambapo toka kikundi hicho kianze mashambulizi katika ardhi ya Uturuki mpaka sasa wameuwawa wanajeshi elfu 40, kwa maana kwamba idadi hiyo ni pamoja na wanamgambo wa kikundi hicho na wanajeshi wa Uturuki.
mwisho wa Habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky