Watu watatu wakamatwa nchini Ujerumani kwatuhuma ya kuwasaidi magaidi wa Ahrar al-Sham

  • Habari NO : 793856
  • Rejea : ABNA
Brief

Wajerumani watatu wakamatwa katika wilaya ya Karlsruhe kwa tuhuma ya kukisaidi kikundi cha kigaidi cha Ahrar al-Sham nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: siku ya Jumanne mahakama ya Ujerumani imetoa taarifa ya kukamatwa kwa watu watatu kwa kosa la kukisaidia kikundi cha kigaidi cha Ahrar al-Sham kinachofanya mauaji ya kikatika kati taifa la Syria.
Majeshi ya usalama nchini Ujerumani yamewatia mbaroni watu hao katika welaya ya Karlsruhe baada ya watu hao kukisaidia kikundi hicho cha Kigaidi nchini Syria, ambapo mmoja kati yao anaumri wa miaka 36 na 39 huku ikibainika kuwa wajerumani hao wana asili ya Syria.
Msaada waliotuma kwa magaidi hao ni pesa, kamera za usalama na vifaa vya mawasiliano vya kisasa ambapo walikipatia kikundi hicho cha kigaidi.
Miaka ya hivi karibuni maelfu ya wananchi wa bala la Ulaya ikiwemo Ujerumani wamekuwa wakienda katika nchi za Iraq na Syria na kujiunga na vikundi vya kigaidi mbalimbali katika nchi hizo, ikiwemo kikundi cha kigaidi cha Daesh na Ahrar al-Sham na kufanya mauaji ya watu wasiokuwa na hatika nchi hizo ikiwemo kuuwa watoto na akinamama.
Kikundi cha Ahrar al-Sham ni katika vikundi vya kigaidi vinavyo pambana na majeshi ya Syria, ambapo kiitikadi wako karibu sana na kikundi cha kigaidi cha Alkaida, magaidi wa Ahrar al-Sham takripa kipo katika mikoa mbalimbali nchini Syria, hususan katika maeneo ya kaskazini mwa hiyo.
mwisho/390


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky