Mwingereza mmoja auwawa kufuatia mapgano yaliotokea Raqqah nchini Syria + picha

  • Habari NO : 802534
  • Rejea : ABNA
Brief

Majeshi ya Kikurdi yaliopo kaskazini mwa mashariki mwa Syria wametangaza kuwa mwingereza mmoja ameuwawa akiwa pamoja na majeshi hayo katika mashambulizi ya kuikomboa mji wa Raqqah nchini Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya wakurdi wanaoishi nchini Syria, wametangaza kuuwawa kwa mwanajeshi ambaye ni Raia wa Uingereza walipokuwa wakipambana na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Televishen ya skynews ya kiarabu imetangaza kuwa wanajeshi wa kikurdi wanaoishi kaskazini mwa mashariki mwa Syria, wametangaza kuuwawa mwanajeshi mmoja wa Uingereza ambaye alikuwa pamoja na jeshi hilo la wakurdi katika shambulio la kutaka kuukomboa mji wa Raqqah nchini humo.
Mwanajeshi huyo wa Uingereza ameuawawa katika vita ya kupambana na kikundi cha kigaidi cha Daesh sehemu ya “Talu Saman” iliopo katika mkoa wa Raqqah nchini humo.
Hii ni katika hali ambayo mapigano makali yamekuwa yakiendelea kati ya majeshi ya Syria na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika vijiji viwili viliopo katika kaskazini mwa mji wa Tabaqah magharibi mwa mkoa wa Raqqah nchini Syria.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky