Watatu wajeruhiwa kwa risasi katika mgahawa nchini Uturuki

  • Habari NO : 802956
  • Rejea : ABNA
Brief

Watu watatu wamejeruhiwa kufuatia shambulio la kurusha risasi katika mgahawa mmoja katika mji mkuu wa Uturuki Istambul.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kwa mara nyingine tena siku ya Jumatano mji wa Istambul umekutwa na mashambulio ya risasi katika mgahawa mmoja nchini humo baada ya watu wenye silaha kufanya shambulio hilo.
Watu wawili waliokuwa na silaha walikuwa wakirusha risasi katika mgahawa mmoja uliopo sehemu ya Fatih katika mji mkuu wa Uturuki Istambul.
Shambulio hilo limepelekea kujeruhiwa mmiliki wa mgahawa huo na wapita njia wawili walikuwa wakipita katika sehemu hiyo, huku watu hao waliokuwa na silaha wakifanikiwa kutoroka katika sehemu hiyo bila ya kujilikana.
Mpaka sasa haijatolewa ripoti yeyote kuhusu washambuliaji hao, pia hawajafahamika wapi walikokimbilia.
Vyombo vya habari vya Uturuki vimetoa ripoti ya kuwa shambulio hilo linahusu ugomvi uliopo baina ya mmliki wa mgahawa na washambuliaji hao.
Siku kadhaa ziliopita mmoja kati ya wanaohusika na kikundi cha kigaidi cha Daesh alishambulia kwa risasi sehemu ya kufanya mazoezi katika nyakati za usiku, shambulio ambalo lilipelekea kuuwawa watu zaidi 40 nchini humo.
Asilimia kubwa ya miji ya Uturuki, hasa mji wa Istambul hivi karibuni imekuwa ikishuhudiwa na mashambulizi mbalimbali ya kigaidi katika mji hiyo na kupelekea kuuwawa mamia ya wananchi wasiokuwa na hatia nchini humo
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky