Muamko wa Kiislamu

Kuzidi wimbi la muamko wa Kiislamu Saudia Arabia

  • Habari NO : 300738
  • Rejea : abna.ir
Ijumaa ilopita Mkoa wa Qatif Saudia Arabia ulishuhudia maandamano makali ya Wananchi wa Mkoa huo kutaka kukamilishiwa mahitaji yao jambo hilo lilipelekea kutiwa mbaroni wa Watu kadhaa katika maandamano hayo.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- inatuarifu kuwa mashariki mwa Saudia Arabia hali si njema kwani wimbi la muamko wa Kiislamu bado la vuma kwa kasi zaidi,  kwa maandamano ya hapa na pale katika Mkoa wa Qatif  Nchini Saudia Arabia, na kulazimika vikosi vya usalama kutia watu kadhaaa mbaroni kwa kosa la kuandamana dhidi ya utawala wa Kifalme wa Ali Saudi.

Maandamano hayo pia yalisababisha Polisi ya Saudia kushika zaidi ya watu 20 kwa kosa la kuandamana, na kupelekea Wananchi wa Mkoa huo kuishi kwa wasi wasi kwani kila akutwae barabarani kutiwa mbaroni bila kosa lolote lile.

Wimbi hili la muamko wa Kiislamu la pelekea utawala wa Ali Saudi kuwa pabaya kwani hatua na mambo yanayofanywa na utawala huo yaelekea ukingoni kwa muamko huo wa Vijana.

Katika vurugu hizo jana alishikwa kijana mwenye umri wa miaka 18 katika Maidan Karamah  katika Mkoa wa Awamiayah, pia alishikwa Jaafar Naghmush katika barabara ya Uhud Mkoa wa Hallah na kupelekwa mahala pasipo fahamika.

Pia waloshikwa Ijumaa ilopita ni Fazil habib Ali Ruqaiyah Mkoani Qatif.

Ijumaa ilopita Mkoa wa Qatif  Saudia Arabia ulishuhudia maandamano makali ya Wananchi wa Mkoa huo kutaka kukamilishiwa mahitaji yao jambo hilo lilipelekea kutiwa mbaroni wa Watu kadhaa katika maandamano hayo.


Mourining of Imam Hossein
بی کفایتی آل سعود
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky