Kuteuliwa Msaidizi mpya wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as)

  • Habari NO : 314735
  • Rejea : Abna.ir
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as) amemtangaza rasmi Hujatul Islam walmuslimin Dr.Najaf Lak Za`ayi kuwa ni msaidizi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as) katika kitengo cha tamaduni katika Jumuiya hiyo, Dr. Najaf Lak Za`ayi ni mmoja kati ya wasambazaji wa mafunzo ya Ahlul Bayt(as) Duniani nanimwana harakati katika Taasisi zote alizokua akieneza mafungo ya Mtume(saw) na kuwa mwenyekuhami Madhehebu ya Shia.

Akhtariy alimuhusia Dr.Najaf Lak Za`ayi kuwa Mchaji Mungu na kuchegemea, nakuwa tayari kueneza mafunzo ya Ahlul Bayt(as) Duniani na kudumisha uhusiano wa Jumuiya na taasisi za kielimu na za uhakiki katika Uislamu.

Na ujumbe wa kuteuliwa kwake ni kama ifuatavyo;

باسمه تعالی

Mheshimiwa Hujatul Islam walmuslimin Dr.Najaf Lak Za`ayi, kutokana na uzowefu ulokuwanao katika sekta tofauti, ndio sababu ya kuteuliwa nakuwekwa kwenye sehemu hii ili kueneza mafunzo ya Ahlul Bayt(as). ambapo Cheo hicho atakuwanacho kwamuda wa miaka mitatu.

Natumai Mwenyezi Mungu atakusaidia na kukufanya kuwa mwenye kumtegemea, na kutekeleza ujumbe wa Kiongozi Muadhamu(Ayatullah sayyid Ali Khamenei) katika kufikisha na kubainisha mafunzo ya Ahlul Bayt(as) na kusaidia Ulimwengu wa Kiislamu na kudumisha umoja baina yao, bila kusahau uhusiano wa taasisi za wahakiki wa Kiislamu na shakhsiah za Wanazuoni katika kuihami Madhehebu ya Kishia, na twatumai kuwa kila hatua utakayo chukuwa itakuwa yenye faida na manufaa kwa jamii inshaallah, nasi twasubiri maendeleo ya Jumuiya hiyo Ahlul Bayt(as) .

nasi twataraji kutoka kwa Mwenyezi Mungu mafaanikio mema.

Muhammad Muhsin Akhtariy

Katibu Mkuu wa Jumjiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as)

 May 2012

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Hujatul Islam walmuslimin Muhammad Muhsin Akhtariy Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as) alitangaza rasmi kuwa Hujatul Islam walmuslimin Dr.Najaf Lak Za`ayi ndie msaidizi mpya wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as) katika kitengo cha mambo ya utamaduni kwa muda wa miaka 3.


بی کفایتی آل سعود
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky