Serikali ya Syria yawaachia huru wafungwa 223

  • Habari NO : 319425
  • Rejea : CRI
Serikali ya Syria imewaachia huru wafungwa 223 huku tukio hilo likishuhudiwa na waangalizi wa Umoja wa Mataifa.

Hayo yamesemwa jana na msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Eduardo Del Buey. Aidha alisema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Nchi za Kiarabu Bw. Kofi Annan walisisitiza mara nyingi kuwa, ni lazima watu wote waliofungwa bila ya sababu za msingi waachiwe huru, hivyo waliitaka Syria iwaachie huru wafungwa wengi zaidi.Habari nyingine zinasema Bw. Annan ambaye yuko ziarani nchini Lebanon jana alisema, rais Bashar al-Assad wa Syria anapaswa kuchukua hatua kadhaa madhubuti, ili kutekeleza mpango wa amani kwa ajili ya kutatua suala la nchi hiyo, ama sivyo hali ya wasiwasi nchini humo itaongezeka.


بی کفایتی آل سعود
پیام امام خامنه ای به مسلمانان جهان به مناسبت حج 2016
We are All Zakzaky