Saudi Arabia yaahidi kutoa msaada kwa raia wa Yemen ambao inawashambulia na ndege za kivita + Picha

  • Habari NO : 684730
  • Rejea : abna.ir
Brief

Ni jambo la kushangaza kwa umoja wa taifa kuomba msaada wa fedha za kuwasaidia wa Yemen wanaodhambuliwa kutoka kwa nchi inayofanya mashambulizi, badala ya kuomba kusimamishwa mashambulizi ambayo yangezuia mauaji hayo.

Saudi Arabia leo imeahidi kutowa msaada wote wa kibinaadamu wa dola milioni 274 uliombwa na Umoja wa Mataifa kuisaidia Yemen ambayo nchi hiyo ndio sababu ya matatizo hayo nchini humo.

 Mfalme Salman wa Saudi Arabia ameamuru kutolewa kwa msaada huo wa kibinaadamu kufuatia ombi la Umoja wa Mataifa hapo Ijumaa la kutaka kupatiwa msaada wa dharura wa dola milioni 274 kwa ajili ya mamilioni ya watu walioathirika na vita na mashambulizi yanayofanywa na Saudia arabia nchini Yemen.

Likikariri taarifa ya serikali shirika la habari la serikali Saudi Press Agency limesema ufalme wa Saudi uko pamoja na ndugu zao wa Yemen na inataraji usalama na utulivu utarudishwa nchini humo.

Umoja wa Mataifa umesema maelfu ya watu wasio na hatia wameuawa na majeshi ya Saudia arabia na wengine wengi kujeruhiwa na maelfu wameyakimbia makazi yao katika uvamizi huo uliofanywa na Saudia arabia nchini humo.

Ni jambo la kushangaza kwa umoja wa taifa kuomba msaada wa fedha za kuwasaidia wa Yemen wanaodhambuliwa kutoka kwa nchi inayofanya mashambulizi, badala ya kuomba kusimamishwa mashambulizi ambayo yangezuia mauaji hayo.

Hii inamanisha kwamba Umoja wa Mataifa unaunga mkono vita na mauaji yanayofanywa na Saudia arabia kwa sharti kwamba waliojeruhiwa na walio athiriwa na vita wapewe misaada ya kibinadamu.

Mashambulizi ya Saudia arabia Yemen


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky