Serikali ya Iran yasema: Haita ruhusu nchi yeyote kuhatarisha maslahi yake Yemen + Picha

  • Habari NO : 687826
  • Rejea : abna.ir
Brief

Saudia arabia inatuhumiwa kwa kutuma mashehe katika nchi za jiran ili kuwashawishi wananchi kujiunga na mapambano dhidi ya Yemen kwa kuwa laghai kuwa, kushiriki vita dhidi ya Yemen ni jihadi.

Naibu Waziri wa mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir Abdollahian, amesema nchi yake na Yemen zimekuwa na maslahi ya pamoja ya kiusalama na haitoruhusu nchi nyengine zenye sauti katika kanda hiyo kuhatarisha maslahi hayo.

 Abdollahian ameliambia leo shirika la habari la Tasnim kuwa watu wengine hawatoruhusiwa kuhatarisha usalama wao katika uwanja wa kijeshi. Waziri huyo ametoa kauli hiyo akizungumzia operesheni ya kijeshi ya mwezi mmoja ya majeshi ya kiarabu yanayoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen.

Wakati huo huo afisa wa Umoja wa Mataifa amesema miundombinu muhimu nchini Yemen, ikiwemo huduma ya kusambaza maji, afya na mawasiliano ya simu iko katika hatari ya kutoweka kutokana na uhaba wa mafuta. Johannes van der Klaauw, amesema huduma zilizopo za afya, maji na chakula zinatoweka haraka kwa sababu mafuta hayapelekwi tena Yemen. Amesema vikwazo vya silaha pia vinasababisha madhara katika utoaji wa misaada ya kibinaadamu.

Saudia arabia inatuhumiwa kwa kutuma mashehe katika nchi za jiran ili kuwashawishi wananchi kujiunga na mapambano dhidi ya Yemen kwa kuwa laghai kuwa, kushiriki vita dhidi ya Yemen ni jihadi.

Wananchi wa Yemen wakiwa tayari kupambana na uvamizi wa Saudia arabia

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky