Mashia wa Nigeria wafanya maandamano kupinga mauaji ya kinyama yaliofanywa na jeshi la nchi hiyo+ picha

  • Habari NO : 724929
  • Rejea : ABNA
Katika mkoa wa Kanu uliopo kaskazini mwa Nigeria kumefanyika maandamo makubwa ya kupinga mauaji ya kinyama yaliofanywa na majeshi ya Nigeria dhidi ya wafuasi wa madhehebu ya Shia katika Mji wa Zaria na kupelekea kuuwawa mamia ya wakazi wa sehemu hiyo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waandamanaji wanao pinga mauaji hayo wamefanya maanfamao katika mkoa wa Kanu kaskazini mwa nchi hiyo.
Katika mkoa wa Kanu uliopo kaskazini mwa Nigeria kumefanyika maandamo makubwa ya kupinga mauaji ya kinyama yaliofanywa na majeshi ya Nigeria dhidi ya wafuasi wa madhehebu ya Shia katika Mji wa Zaria na kupelekea kuuwawa mamia ya wakazi wa sehemu hiyo.
Waandamanaji hayo nchini humo wamekemea vikali kitendo walichokifanya majeshi ya nchi hiyo dhidi ya wafuasi wa madhehebu ya kishia, huku wakisisitiza kuwa vitendo kama hivyo havitaweza kuzua kutetea haki nchini humo.
Majeshi ya nchi hiyo asubuhi ya siku ya Jumapili yalivamia nyumba ya Sheikh Ibrahimu Zakizaki wakikusudia kumkamata sheikh huyo, katika uvamizi huo majeshi ya serikali ya Nigeria yalitumia risasi za moto kuwapiga wananchi waliokuwa wanazuia kukamatwa kwa Sheikh huyo na kusababisha vifo vya watu wengi waliokuwa katika nyumba ya Sheikh huyo.
Baadhi ya vyanzo vya habari vinaarifu kuwa shambulio hilo limesababisha kuuwawa viongozi wa hali ya juu wa kikundi cha harakati ya kiislamu nchini humo, ambao miungoni mwao ni Sheikh Muhammad Turiy, DK Mustafa Saidi, Ibrahimu Athumani na Juma Galima, ambao kwamba kinidhamu ndio wanao fuata baada ya Sheikh Zakizaki.
Aidha katika shambulio hilo pia Zainab Ibrahim mke wa Sheikh Zakizaki na Sayyed Ali Zakizaki ambaye ni mtoto wake ni katika waliofariki katika tukio hilo la kusikitisha.  


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky