Maandamano ya mashia nchini Nigeria yavamiwa na kupigwa vibaya na Polisi wa nchi hiyo

  • Habari NO : 725157
  • Rejea : ABNA
Brief

Jeshi la polisi nchini Nigeria limeshambulia waandamanaji wa madhehebu ya kishia nchini humo, ambayo yamefanyika katika mikoa ya kaskazini mwa nchi hiyo, ikiwa ni katika hali ya kupinga mauaji ya kikatilili ya Mashia wa nchi hiyo, pia maandamano hayo kupelekea idadi kadhaa ya waandamanaji kuuwawa na wengine kujeruhiwa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kwa mara nyingine tena waumini wa dhehebu la Shia nchini Nigeria wahujumiwa kutokana na vitendo visiokuwa vya kibinadamu ya majeshi ya nchi hiyo.
Jeshi la Polisi la nchi hiyo limeshambulia waandamanaji katika mkoa wa Kanu kaszkazini mwa nchi hiyo na kuwapinga vibaya waandamanaji hao, huku msemaji mkuu wa taasisi ya kiislamu nchini humo ametangaza kuwa katika mashambulizi hayo yaliofanywa na jeshi la Polisi yamepelekea kuuwawa watu watatu na makumi mengine kujeruhiwa, pamja kuwa kutokana na hali mbaya waliokuwa nayo majeruhi hao yawezekana ikaongezeka idadi ya vifo katika masaa ya usoni.
  Mashambulizi ya Polisi hao dhidi ya waandamanaji hao yametokea katika mkoa wa Kaduna, katika hali ambayo maandamano mengine yaliofanyika katika wilaya ya nyingine yalifanya kwa amani na utulivu bila ya kufanyiwa hujuma yeyote.
Wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano makubwa katika pande mbalimbali za nchi hiyo kupinga mauaji ya kinyama waliofanyiwa wafuasi wa madhehebu ya Shia nchini humo, huku wakiomba serikali ya Nigeria kumwacha huru kiongozi wa mashia nchini humo.
Mashambulio yaliofanywa na majeshi ya Nigeria dhidi ya wafuasi wa madhehebu ya kishia nchini humo katika nyumba ya Sheikh Zakzak na makao makuu ya taasisi ya harakati ya kiislamu nchini humo yamesababisha kufariki mamia ya watu na wengine wengi kujeruhiwa.
mwisho wa Habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky