Mazishi ya Kamanda wa Hizbullah aliyeauawa na Israel, Hizbullah yaahidi kulipa kisasi

  • Habari NO : 726237
  • Rejea : abna.ir
Brief

Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa: Hapana shaka kwamba Hizbullah inahaki ya kulipa kisasi na italipa kisasi kwa muda inaotaka, mahali inapotaka na namna itakavyotaka.

Shirila la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kamanda wa Hizbullah aliyeuawa katika shambulizi lililofanywa na ndege za kivita za Israel nchini Syria, amezikwa leo katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

Maelfu ya wananchi, viongozi mbali mbali wa nchi, wanasiasa walishirikiana sanjari na wanajeshi wa Hizbullah katika mazishi ya kamanda huyo.

Vikundi ya wapiganaji wa Kipalestina vimeahidi kulipa kisasi kufuatia kifo cha kamanda huyu wa Hizbullah ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi madhulumu wa Palestina.

Shahidi Samir Qantwar amezikwa katika makaburi ya mashahidi ya Hadharat Zainab mjini Beirut, mahala ambapo mashahidi na wapiganaji wa Hizbullah huzikwa.

Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Hizbullah alipokuwa katika mazishi hayo alisema : Samir Qantwar alikuwa anatafuta kitu chenye thamani kuliko kuachwa huru kutoka gerezani, Samir Qantwar alikuwa anataka kufa kishujaa akitetea dini na maslahi ya uislamu na nchi yake, na kwa hakika kwa kifo chake amefikia malengo aliyokuwa akitaka kuyafikia, Shahidi Samir Qantwar aliumbwa kwa ajili ya kutetea ardhi zilizoporwa na Israel na amefariki akitetea ardhi hizo.

Sayyid Swafaddin alimalizia kwa kusema: Kama Israel imeshindwa kujifunza kutokana na makosa yake ya awali ya kuwaua viongozi wa Hizbullah, sasa hivi watafahamu kwamba wamefanya ujinga watakao ujutia daima kwa kumuua Samir Qantwar.

Ramadhan Sharif ambaye ni Jeneral wa jeshi la Iran: amesema kuwa: kifo cha Samir Qantwar kimeongoza ari na mori kwa wanajeshi wa Hizbullah wa kuendeleza mapambano dhidi ya Israel.

Jeneral Ramadhani ameeleza kuwa kitendo cha Israel kuwasaidia magaidi wanaopambana dhidi ya Syria na kitendo cha kufanya mashambulizi dhidi ya makanda wa Hizbullah hakiwezi kufumbiwa macho hata kidogo.

Kiongozi mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah amesema: Israel imemuua kamanda Samir Qantwar, sasa ni zamu ya Hizbullah kujibu uchokozi huo.

Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa: Hapana shaka kwamba Hizbullah inahaki ya kulipa kisasi na italipa kisasi kwa muda inaotaka, mahali inapotaka na namna itakavyotaka.

Serikali ya Israel imewaambia wananchi wake wakae kwenye mahandaki mpaka hali ya utulivu itakapotangazwa.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky