Umoja wa Ulaya wajipanga kuisaidia Libya

  • Habari NO : 748517
  • Rejea : abna.ir
Brief

Umoja wa Ulaya ambao ulishiriki katika kusababisha machafuko nchini Libya unapanga kuisaidia serikali mpya ya nchi hiyo baada ya kuanguka utawala wa Muammar Gaddafi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Umoja wa Ulaya ambao ulishiriki katika kusababisha machafuko nchini Libya unapanga kuisaidia serikali mpya ya nchi hiyo baada ya kuanguka utawala wa Muammar Gaddafi.

Maziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanatafuta njia za kuisaidia serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya, na pia kujadili namna ya kudhibiti uhamiaji haramu kutoka taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond ndiye afisa wa hivi karibuni wa Umoja wa Ulaya, kuzuru Libya hii leo baada ya wenzake kutoka Ujerumani na Ufaransa kufika nchini humo mwishoni mwa juma katika juhudi za kuunga mkono utawala wa Waziri Mkuu mteule Fayez Serraj.

Hammond alipelekwa chini ya ulinzi mkali hadi katika kambi ya kijeshi, ambako utawala wa Waziri Mkuu Fayez Serraj unajaribu kujiimarisha. Waziri Hammond amesema nchi yake inaunga mkono mikakati ya kurejesha amani na uthabiti katika taifa zima la Libya, huku akitangaza dola milioni 14 za kuisaidia serikali mpya kuimarisha taasisi za kisiasa, uchumi, usalama na haki.

Uingereza kutoa mafunzo kwa vikosi vya Libya iwapo msaada huo utahitajika

Mataifa ya Magharibi yanatumai kuwa serikali mpya ya Libya itawaunganisha walibya wote na kuisaidia nchi hiyo kupambana na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh ambao walikuwa wakiunga mkono na nchi za Ulaya kipindi cha kupambana na utawala wa Muammar Gaddafi. Aidha maafisa wa Uingereza wamesema nchi hiyo iko tayari kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Libya juu ya namna ya kukabiliana na kundi hilo lililo na itikadi kali. Hata hivyo maafisa hao hawakuweka wazi taarifa kwamba kuna njama ya maelfu ya wanajeshi wa Magharibi kupelekwa nchini Libya, hivi karibuni.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, amesema serikali mpya inapaswa kuanza kufanya kazi vizuri na kwamba ni jukumu la Umoja wa Ulaya kuipa serikali hiyo kila nafasi ya kuweza kufanikiwa.

Mawaziri hao wa mambo ya nje kutoka mataifa 28 ya Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri Mkuu mteule Serraj baadaye hii leo jioni.

Libya ilitumbukia katika mapigano baada ya kuuwawa kiongozi wake Muammar Gadhafi mwaka wa 2011, hali iliyotoa nafasi kwa wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh au  dola la kiislamu kujiimarisha huku serikali mbili hasimu zikipigania uongozi, moja iliyoko mjini Tripoli inayoungwa mkono na wanamgambo na nyengine Mashariki mwa Libya inayotambuliwa Kimataifa.

Mwisho wa habari/ 291

 


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky