Hatimae kiongozi wa waasi awasili Sudan

  • Habari NO : 750104
  • Rejea : abna.ir
Brief

Riek Machar amerejea Juba kujiunga na serikali ya umoja wa taifa iliyolengwa kumaliza zaidi ya miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mkuu wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar hatimaye amewasili Juba na kuhimiza watu washirikiane. Riek Machar amerejea Juba kujiunga na serikali ya umoja wa taifa iliyolengwa kumaliza zaidi ya miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe."Tunabidi tuwalete pamoja watu wetu,ili waungane na kuponya majaraha" alisema  Machar aliyepokelewa na mawaziri na wanadiplomasia alipowasili uwanja wa ndege. Mara baada ya kuwasili Riek Machar amepangiwa moja kwa moja kwenda ikulu kuapishwa kama makamo wa rais . Riek Machar alikuwa akisubiriwa kuwasili Juba tangu April 18 iliyopita,kukawia kwake mara kadhaa kulizusha hofu makubaliano ya amani yangeingia hatarini. Kiongozi wa wa kijeshi wa waasi Simon Gatwech Dual amerejea Juba jumatatu katika kile kinachoangaliwa kama hatua mojawapo muhimu ya kuunusuru mpango wa amani.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky