Ufaransa: Boko Haram bado ni kitisho cha usalama

  • Habari NO : 754420
  • Rejea : abna.ir
Brief

Ikumbukwe kuwa Jeshi la Nigeria katika masiku yaliyopita limevamia kundi la waislamu wa dhehebu la Shia ambao hawakuwa na silaha na kufanya mauaji ya halaiki, ambapo mpaka sasa jeshi hilo limeshindwa kutoa maelezo ya jinai hizo ilizofanya huku rais wa Nigeria akiendelea kuwa kimya.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema Boko Haram bado ni kitisho licha ya hatua za kuridhisha za kijeshi zilizochukuliwa kuliangamiza kundi hilo la kigaidi lenye ngome yake nchini Nigeria.

Akizungumza katika mkutano wa kilele kujadili kitisho hicho cha Boko Haram mjini Abuja, Nigeria, Hollande amesema matokeo ya operesheni dhidi ya Boko Haram ni ya kuridhisha kwani magaidi hao wamekatwa makali na kulazimika kurudi nyuma.

Nigeria ni mwenyeji wa mkutano huo wa kilele wa kujaidli kitisho kinachosababishwa na uasi huo wa Boko Haram, mkutano unaowaleta pamoja viongozi wa Ufaransa, Cameroon, Niger, Benin na Niger.

Na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Philiph Hammond, naibu wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken, maafisa wa jumuiya za Afrika magharibi na kati na maafisa wa Umoja wa Ulaya.

Miaka saba ya uasi kaskazini mashariki mwa Nigeria, imesababisha mauaji ya watu takriban 20,000 na kuwaacha wengine milioni 2.6 bila ya makaazi na kusababisha mzozo wa kibinadamu.

Boko haram kama ilivyo makundi mengine ya kigaidi yanafuata misimamo ya kidini ya siasa kali kutoka Saudia arabia.

Boko Haram ikabiliwe vipi?

Mazungumzo katika mkutano wa kilele wa usalama unatarajiwa kuangazia kutumwa rasmi kwa kikosi cha wanajeshi wa nchi za kanda hiyo ya magahraibi mwa Afrika kinachohusisha Nigeria na majirani zake kukabiliana na Boko Haram.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake kuhusu mafungamano kati ya kundi hilo la Boko Haram na kundi la wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh wenye itikadi kali  zinazosabazwa toka Saudia arabia , baada ya ripoti kuwa kuna wapiganaji wa kutoka Nigeria wanaopigana vita vya wanavyodai kuwa ni jihadi nchini Libya.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa mafungamano hayo ni kitisho kwa usalama barani Afrika.

Baraza la usalama hapo jana Ijumaa limesema mazungumzo ya Abuja yanapaswa kuunda mkakati madhubuti wa kushughulikia uongozi, usalama, maendeleo na usaidizi wa kiuchumi, kijamii na kibinadamu kuushughulikia mzozo uliosababishwa na uasi wa Boko Haram katika kanda hiyo.

Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau mwaka jana alitangaza kuwa mtiifu kwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Daesh Abu Bakr Al Baghdad. Ufaransa imetoa mafunzo na vifaa kama sehemu ya juhidi za kimataifa za kuisaidia Nigeria kukabiliana na Boko Haram. Hollande na Buhari wametia saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili.

Hammond pia ameonya kuwepo kitisho kikubwa kutokana na mafungamano ya Boko Haram na kundi la kigaidi la Daesh lakini amesema kuna ufanisi katika kukabiliana na makundi hayo kufuatia usaidizi kutoka kwa Ufaransa, Uingereza na Marekani.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Uingereza amesema huu sio wakati wa kulegeza kamba katika vita dhidi ya Boko Haram na kuna haja ya kurejesha uthabiti katika kanda hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Mkutano huo wa kilele, unakuja miaka miwili baada ya mwingine wa ngazi ya juu kufanyika Paris. Jeshi la Nigeria limekuwa likipambana vikali na waasi wa Boko Haram katika siku za hivi karibuni katika msitu wa Sambisa ambao ni ngome ya waasi hao.

Je Buhari atawaangamiza waasi?

Rais Buhari ameapa kulishinda kundi hilo kabla ya kumaliza mwaka mmoja tangu aingie madarakani. Jeshi la Nigeria limetangaza kundi hilo linasambaratika. Hata hivyo naibu wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken amesema haionekani kama Boko Haram limeshindwa.

Kutumwa kwa kikosi cha wanajeshi 8,500 wa kikanda kitakachojumuisha wanajeshi kutoka Nigeria, Benin, Cameroon, Chad na Niger kunatarajiwa kuwepo miongoni mwa ajenda kuu za mkutano huo.

Kikosi kinachoungwa mkono na Umoja wa Afrika kilicho na makao yake katika mji mkuu wa Chad, N'djamena kilipaswa kuanza kufanya operesheni dhidi ya Boko Haram mwezi Julai mwaka jana.

Boko Haram imetanua mashambulizi yake nje ya Nigeria, na mara kadha imezishambulia, Cameroon, Niger na Chad. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power amesema watu milioni 9.2 katika nchi hizo wameathirika na mzozo huo.

Ikumbukwe kuwa Jeshi la Nigeria katika masiku yaliyopita limevamia kundi la waislamu wa dhehebu la Shia ambao hawakuwa na silaha na kufanya mauaji  ya halaiki, ambapo mpaka sasa jeshi hilo limeshindwa kutoa maelezo ya jinai hizo ilizofanya huku rais wa Nigeria akiendelea kuwa kimya.

Mwisho wa habari/ 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky