Jeshi la Nigeria ladai kuokoa wanafunzi 96 wa Chibok waliotekwa na Boko haram

  • Habari NO : 755371
  • Rejea : abna.ir
Brief

Jeshi la Nigeria limedai kuwaokoa baadhi ya wanafunzi wakike waliotekwa na wafuasi wa kundi la kigaidi la Bokoharamu.

 Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Jeshi la Nigeria limedai kuwaokoa baadhi ya wanafunzi wakike waliotekwa na wafuasi wa kundi la kigaidi la Bokoharamu.

 Wanaharakati wanaopigania kukombolewa wanafunzi zaidi ya 200 waliotekwa nyara na Boko Haram miaka zaidi ya miwili iliyopita wanatilia shaka ripoti zilizotangazwa na jeshi kwamba  mwanafunzi wa pili wa Chibok ameokolewa. Jeshi lilitangaza jana kuwaokoa jumla ya wanawake na watoto 97 wiki hii, akiwemo mwanafunzi  mwengine wa Chibok. Jeshi limemtaja msichana huyo kuwa ni Serah Luka aliyekuwa akiishi Madagali, mji mmoja wa jimbo la Adamawa jirani na jimbo la Borno. Hata hivyo, Auwa Biu wa kundi la wanaharakati wanaodai kukombolewa wanafunzi wa Chibok anasema katika orodha yao hawakukuta jina kama hilo. Wanasema hata hivyo pengine jina lake limeandikwa vibaya. Makundi mengine pia ya wanaharakati yalidai hapo awali kutilia shaka maelezo yaliyotolewa na jeshi. Jeshi la Nigeria limemkomboa mwanafunzi wa kwanza wa Chibpok jumanne iliyopita. Amina Ali Darsha Nkeki alikaribishwa na rais Muhammadu Buhari jana aliyesema anaamini na wanagfunzi wengine pia wa Chibok watakombolewa.

Mwisho wa habari/ 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky