Rais wa Tanzania amtimua kazi waziri mlevi

  • Habari NO : 755571
  • Rejea : abna.ir
Brief

Tanzania inatarajiwa kuwa ni nchi yenye maendeleo ya kasi ya ajabu katika nchi za Afrika, kutokana na juhudi za rais Pombe magufuli ambaye ni zao la rais mstaafu Dk Mrisho Jakaya Kikwete, ambaye ni moja katika watu walimuunga mkono na hatimaye kufanikisha kuingia madarakani rais Magufuli.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa  jamhuri ya Muungano wa Tanzania dk: John Pombe Magufuli amemfuta kazi waziri wake wa mambo ya ndani baada ya waziri huyo Charles Kitwanga, kuingia bungeni na kijibu maswali huku akiwa amelewa. Kitwanga ndiye waziri wa kwanza kufukuzwa kazi na rais Maguli tangu alipounda baraza lake la mawaziri, lakini wachambuzi wamesema kutimuliwa kwake kumekuja kama mshangao kwa sababu alikuwa akitazamwa kama mtu wa karibu zaidi na Magufuli.

Taarifa ya kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu ilisema hapo jana kuwa Kitwanga alifukuzwa kwa sababu ya kuingia bungeni na kujibu maswali yaliolekezwa kwa wizara ya mambo ya ndani akiwa amelewa. Rais Magufuli ambaye aliingia madarakani mwezi Novemba, aliahidi kupambana na ufisadi na uzembe serikalini. Tayari amewafuta kazi maafisa kadhaa waandamizi kwa tuhuma za rushwa na kupunguza matumizi ambayo anayaona kuwa ya ubadhirifu.

Rais Magufuli ni miongoni amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na utendaji kazi wake ulio na umakini wa hali ya juu kutokana na kupambana vikali na ufisadi na kufanya juhudi za kuondoa tofauti kati ya masikini na matajiri.

Juhudi za pekee za rais huyo zinapokelewa tofauti ambapo wananchi wengi hasa wenye maisha magumu wanamuunga mkono rais huyo, lakini wengi wa wapinzani wake na baadhi ya wananchi wanaofuata fikra za wapinzani wamekuwa wakikosoa juhudi za rais huyo, lakini pia wapo wapinzani wanaomkosoa kwa kutumia mantiki.

Tanzania inatarajiwa kuwa ni nchi yenye maendeleo ya kasi ya ajabu katika nchi za Afrika, kutokana na juhudi za rais Pombe magufuli ambaye ni  zao la rais mstaafu Dk Mrisho Jakaya Kikwete, ambaye ni moja katika watu walimuunga mkono na hatimaye kufanikisha kuingia madarakani rais Magufuli.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky