Serikali ya Misri yatuma meli za kijeshi kutafuta ndege ya Egypt Air iliyoanguka baharini + Picha

  • Habari NO : 755746
  • Rejea : abna.ir
Brief

Serikali ya Misri imetuma nyambizi katika jitihada za kukitafuta kisanduku cha mawasiliano cha ndege ya abiria ya EgyptAir,

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Misri imetuma nyambizi katika jitihada za kukitafuta kisanduku cha mawasiliano cha ndege ya abiria ya EgyptAir, iliyoanguka katika bahari ya Mediterenia Alhamisi iliyopita. Kisanduku hicho kinatarajiwa kubainisha chanzo cha kuanguka ndege hiyo. Rais wa Misri Abdel fattah el-Sissi amesema ni mapema mno kujua kipi kilosabbashia ndege ya chapa AirBus A320 kuanguka ikiwa imebeba abiria 66. Msemaji Mkuu wa wizara ya safari za anga ya Misri amesema baadhi ya mabaki ya ndege hiyo iliyokuwa njiani ikitoka Paris kuelekea mji mkuu wa Misri Cairo yamepatikana, lakini maiti za abiria bado hazikupatikana. Sisi amesema hadi sasa hakuna sababu zinazoweza kuthibitishwa.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky