Jeshi Niger lauwa magaidi wa Boko Haram 12

  • Habari NO : 757081
  • Rejea : abna.ir
Brief

Maafisa usalama nchini Niger wamewauwa wapiganaji 12 kutoka kundi la kigaidi la Boko Haram, ambao walifanya shambulizi kusini/mashariki mwa eneo la Bosco liliopo karibu na mpaka wa taifa hilo na Nigeria

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Maafisa usalama nchini Niger wamewauwa wapiganaji 12 kutoka kundi la kigaidi la Boko Haram, ambao walifanya shambulizi kusini/mashariki mwa eneo la Bosco liliopo karibu na mpaka wa taifa hilo na Nigeria. Msemaji wa jeshi kanali Moustapha Ledru amesema wanajeshi wa tatu wa taifa hilo wamejeruhiwa wakati wa mapigano na kwamba jeshi limefanikiwa kuteka kutoka kwa maadui zao baadhi la silaha zikiwemo bunduki ana ya rashasha,mizinga pamoja na simu za mkononi. Bosco iko katika jimbo la Diffa, ambayo umetoa hifadhi ya wakimbizi wa nje na wa ndani ya Niger waliokimbia madhila ya Boko Haram. Eneo hilo limekumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara yenye kuhusishwa na wapiganaji hao wenye itikadi kali za Kiislamu zinazotoka Saudia arabia.

Mwisho wa habari / 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji
We are All Zakzaky